4 Novemba 2025 - 12:21
Sayyid Ali Khomeini: “Kama Ubalozi wa Marekani usingelivamiwa, leo tusingekuwa na Makombora wala ishati ya nyuklia"

Akiisisitizia kauli kwamba “uvamizi wa ubalozi wa Marekani uliimarisha uhuru wa Iran,” alisema: “Kama tukio hilo lisingetokea, leo hii Jamhuri ya Kiislamu isingekuwepo, na nchi yetu isingepata teknolojia ya makombora na nishati ya nyuklia, kwani Marekani ilikuwa inapinga maendeleo haya.”

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-, Sayyid Ali Khomeini, mjukuu wa Mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Al-Marhumu Imam Khomeini (MA), amesema kuwa kama ubalozi wa Marekani usingelivamiwa mwaka 1979 (1358 kwa kalenda ya Kiirani), leo hii kusingekuwepo Jamhuri ya Kiislamu, wala Iran isingefikia teknolojia ya kujihami na ya nyuklia. Ameeleza tukio hilo kuwa ni “mapinduzi ya pili” yaliyoihakikishia Iran uhuru wake.

Kwa mujibu wa shirika la habari Khabari la ABNA, Sayyid Ali Khomeini, katika hotuba yake kwa mnasaba wa kumbukumbu ya uvamizi wa ubalozi wa Marekani, alisema: “Watu wa Iran, miaka hamsini iliyopita, walikuwa kitu kimoja nyuma ya wanafunzi waliouvamia ubalozi wa Marekani, kwa sababu walitaka kuthibitisha kuwa inawezekana kusimama dhidi ya nguvu za ulimwengu.”

Akiisisitizia kauli kwamba uvamizi wa ubalozi wa Marekani uliimarisha uhuru wa Iran,” alisema: “Kama tukio hilo lisingetokea, leo hii Jamhuri ya Kiislamu isingekuwepo, na nchi yetu isingepata teknolojia ya makombora na nishati ya nyuklia, kwani Marekani ilikuwa inapinga maendeleo haya.”

Sayyid Ali Khomeini aliongeza: “Nchi nyingi za eneo hili haziruhusiwi hata kuwa na ulinzi wa anga kwa sababu Marekani inasema zisiwe nazo. Kama mtazamo wa wakati ule ungeendelea, nasi leo tusingekuwa na makombora, ulinzi wa anga, wala nishati ya nyuklia.

Mjukuu huyo wa Imam Khomeini aliendelea akisema: “Kwa mujibu wa tafsiri ya Imam kuhusu tukio la tarehe 13 Aban, uvamizi wa ubalozi wa Marekani ulikuwa mapinduzi makubwa zaidi kuliko Mapinduzi ya Kwanza; mapinduzi yaliyoihakikishia Iran uhuru wake na kuhuisha roho ya kujitegemea ndani ya taifa.”

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha